Komamanga ni tunda lenye asili ya India na Persia kwa jina la kisayansi ni Punica Granatum, lakini lililetwa Marekani na wawekezaji wa Kihispania na kwa sasa limejulikana dunia nzima.
Tunda hili hustawi sana kipindi cha mwezi wa tisa na wapili, na huweza kushamiri sana katika hali ya hewa ya joto, lakini pia komamanga ni hodari katika kumudu hali ya ukame.
Kama hujawahi kula komamanga huwezi jua nini unakosa, lakini ukweli ni kwamba komamanga sio tunda tu bali ni chakula kilichojawa na afya ya vitamin, madini pamoja na virutubisho vingine vingi vinavyoweza kufanya miili yetu kuwa na afya na nguvu tele.
Tunda hili pia linajulikana kama ‘Granada’ au Tufaa la kichina (Chinese Apple), hali kadhalika tunda hili hufahamika zaidi kwa uzuri wa juisi yake.
Mkomamanga huweza kukua kwa urefu wa mita 5 hadi 8 na ina uzito wa gram 200, huku ikiwa na ‘calories’ za kutosha. Ambapo katika gram 100 komamanga huweza kutupatia kiasi cha 83 ‘calories,’ pia tunda hilo linaelezwa kutokuwa na ‘cholesterol’ wala mafuta.
VIRUTUBISHO VINAVYOPATIKANA KATIKA KOMAMANGA
●Lina vitamin C kwa wingi
●Vitamin B5
●Vitamin A
●Vitamin E
●Madini kama Potassium na Iron
●Mbegu zake ni chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi
‘fiber’
KAZI ZAKE MWILINI
●Unywaji wa juisi ya mbegu za komamanga utakupa dozi kamili ya kansa, pia husaidia mtiririko wa damu kwenda vizuri katika mishipa ya damu, ambayo husaidia presha ya damu na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kiharusi.
●Hulinda meno kuzuia kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu, bakteria na maambukizi ya virusi ndani ya mwili, lakini pia husaidia kutibu madhaifu ya tumbo kama kuharisha, kutopata choo na maambukizi mbalimbali, matatizo sugu ya gesi tumboni hasa vidonda vya tumbo, hupunguza tindikali tumboni n.k
Huko nyuma pia uchunguzi ulionyesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na antioxidant nyingi na vitamini mbalimbali, ambazo hulifanya tunda hilo liweze kusaidia katika mapambano dhidi ya magonjwa ya saratani, matatizo ya moyo na hata ugonjwa wa kusahau uzeeni au Alzheimer.
Inasemekana kwamba ukinywa juisi ya komamanga (pomegranate) nusu lita kila siku kwa muda wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza mafuta tumboni kwa wale wenye vitambi.
KWA WANAUME:
Tunatoa mwongozo wa kurudisha nguvu za kiume, kuongeza uzalishwaji wa mbegu kiume, ni somo kamili utakalolifanya wewe mwenyewe na siyo kumeza dawa.Gharama ni Tsh 5,000/= tu kwa mwongozo mzima, niachie ujumbe 0622925000 whatsapp kwa huduma hiyo ili tusaidiane kurudisha heshima kwenye ndoa/mahusiano yetu
Unaweza like page yetu facebook “kona ya afya kupitia mimea”
na pia share zaidi makala hii ili watu wengi zaidi wajifunze kuhusu
tiba hizi za vyakula na kujipatia makala nyingi katika page na blog yetu
kila siku
Thanks
LikeLike