Kwa ufupi:
Maboresho ya Serikali za Mitaa Tanzania yamelenga katika utoaji bora wa huduma wa Serikali za Mitaa kwa kuzingatia
sera za kitaifa za Serikali Kuu. Maboresho yamekaribisha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, washirika wa maendeleo na wadau wengine tangu awamu ya kwanza hadi sasa. Sera ya Ugatuaji wa
Madaraka (D by D) iliwekwa dhahiri mwaka 1998 na utekelezaji wake wa maboresho ya Serikali za Mitaa ulianza
mwaka 2000. Kupitia ushirikiano huu maboresho ya Serikali za Mitaa hapa Tanzania yamefanikiwa kuleta Serikali za
Mitaa za kidemokrasia, matumizi bora ya raslimali watu, kuongozeka kwa ruzuku toka hazina, kuimarika kwa utawala
bora katika Serikali za Mitaa, kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi, na kwa ujumla kuongezeka kwa uhuru wa serikali
za mitaa katika utoaji huduma.