Kwa ufupi:
Uzalishaji wa mboga mara nyingi unahusisha matumizi ya viuatilifu vyenye kemikali. Wakulima baadhi hawawezi kumudu gharama kubwa za viuatilifu hivi, ambavyo visipotumika vizuri – huweza kuleta madhara, kama kuharibu mazingira, mimea na kuathiri watumiaji wa mboga. SEVIA pia inahamasisha njia za asili katika kupambana na wadudu sumbufu na magonjwa bila kemikali.