Kwa ufupi:
FARM Africa ni shirika lisilo la kiserikali, na shughuli zake nyingi zimejikita kati kuchangia
kupunguza umaskini wa Mtanzania wa hali yachini. Shirika hili linafanya shughuli zake
zaidi katika Wilaya zaBabati, Mbulu na Hanang, mkoani Manyara.
Kwa miaka mingi sasa shirika limeona umuhimuwa kuwekeza katika elimu kwa kuamini
kuwa ni moja kati ya njia zinazoweza kusaidia kupunguza umasikini kama ikiboreshwa na
kutolewa kwa uhakika.
FARM Africa, inaamini kuwa, pamoja na masomo ya nadharia, ni muhimu pia wanafunzi
wakipatiwa elimu ya vitendo ambayo itawawezesha wanafunzi walio wengi kupanua ujuzi
wa kawaida walio nao tayari au kuwaongezea ujuzi mpya kabisa. Kwa kupata ujuzi huo,
wengi wao wataweza kuutumia katika kuboresha maisha yao baada ya kumaliza shule.
Kwa kuona umuhimu huo kupitia somo la stadi za kazi, FARM Africa iligundua upungufu
wa vitabu vwa kufundishia na ndipo uamuzi wa kuandaa na kuchapisha kitabu hiki
ulipojitokeza, Kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vingine sita ambavyo vimeshachapishwa
katika harakati za kusaidia ufundishaji wa somo la stadi za kazi.