xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.contributor.author | Wanafunzi wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA | |
dc.date.accessioned | 2023-02-27T09:07:03Z | |
dc.date.available | 2023-02-27T09:07:03Z | |
dc.date.issued | 2022 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/671 | |
dc.description.abstract | Korosho ni zao la biashara linaloweza kudumu kwa muda mrefu. Mti wa mkorosho huanza kutoa mavuno ifikapo miaka mitatu hadi minne baada ya kupandwa. Kadri umri wa mkorosho unavyo ongezeka, ndivyo mavuno yanavyoongezeka ya. Kiwango cha juu cha mavuno hupatikana mkorosho unapofikia umri wa miaka saba hadi 10, na baada ya miaka 10 mavuno huanza kupungua. Mti wa mkorosho huhitaji eneo la kutosha ili kuruhusu ustawi na kuongeza kiwango cha mavuno. Mti wa mkorosho hustawi zaidi ukanda wa joto. Mikoa inayozalisha zaidi korosho ni Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, na Ruvuma. Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na vituo vya utafiti ikiwamo Naliendele, mikoa mingine inayofaa kwa uzalishaji ni Morogoro, Singida, Iringa, Dodoma na Mbeya. Zao la korosho lina faida nyingi, zikiwemo; hutumika kama chakula na kuzuia mmomonyoko wa udongo, na malighafi ya viwandani kwani korosho ni chanzo cha mafuta inapopogolewa. Vile vile zao la korosho ni chanzo cha ajira cha kuongeza kipato kwa mkulima, hivyo kumwezesha kuboresha maisha, mfano kujenga nyumba bora na kusomesha watoto na kinaongeza pato la taifa kwani ni chanzo cha pesa za kigeni Kijitabu hiki kimeandaliwa kwa ajili ya kumsaidia mkulima kuweza kufahamu kuhusu namna ya uzalishaji bora wa korosho kuanzia zikiwa shambani mpaka sokoni, ili kuweza kufikia matarajio yaliyo bora katika uzalishaji wa zao hilo. Hivyo ni matarajio yetu kuwa, kupitia kijitabu hiki, mkulima wa zao la korosho ataweza kutambua mbinu bora za uzalishaji wa zao la korosho. | en_US |
dc.publisher | Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo | en_US |
dc.subject | Korosho | en_US |
dc.subject | Zao la biashara | en_US |
dc.title | Mwongozo wa kilimo cha zao la korosho: | en_US |
dc.title.alternative | kwa wakulima wadogo Tanzania | en_US |
dc.type | Article | en_US |