Kwa ufupi:
Minjingu ni mbolea asilia ya kupandia.
Mbolea hii inatokana na miamba
inayochimbwa katika eneo la Minjingu
mkoani Manyara ambayo husagwa na
kufungashwa kwenye kiwanda
kilichojengwa katika eneo hilo. Mbolea ya
Minjingu ina kirutubisho cha mimea aina
ya fosiforasi kati ya asilimia 12.3-13.2.
Tofauti na mbolea nyingine za kupandia
zenye madini ya fosiforasi kama vile TSP
na DAP ambazo huagizwa nje ya nchi
hivyo kugharimu fedha nyingi za kigeni,
mbolea hii inayopatikana hapa nchini bei
yake ni nafuu