Kwa ufupi:
Kitabu hiki kina sura saba ambazo zinaangalia sera mabali mbali kuhusu maendeleo vijijini na mchango
wake kwenye kupunguza umaskini Tanzania. Kinaanza na sera zilizotungwa na kuetekelezwa kipindi cha
Ujamaa na Kujijetegemea. Kina sura nyingine zinazo angalia mchango wa elimu kwenye ufanisi wa kilimo;
mradi wa matrekta madogo aina ya ‘power tillers’ kwenye baadhi ya wilaya; awamu tatu za sera za ruzuku
za pembejeo kwa wakulima wadogo; na kilimo cha tumbaku na hatima yake kutokana na mabadiliko
kwenye soko na sera za kimataifa kuhusu zao hilo. Pia kuna sura moja inayolinganisha mbinu za ukuzaji
mnyororo wa thamani kwenye zao la korosho nchini Tanzania na Vietnam na nyingine ambayo inagusia
mambo muhimu ya kufanikisha ushirikiano kati ya taasisi za kiserikali na asisi zisizo za kiserikali katika
kutekeleza na kufanikisha sera za kilimo nchini Tanzania