Kwa ufupi:
Nchini Tanzania zao la nyanya hulimwa karibu katika mikoa yote hasa ya Arusha, Kilimanjaro,
Morogoro, Iringa, Mwanza, Dodoma, Tanga, Pwani na Mbeya. Nyanya ni zao la chakula na
biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana
haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili,
wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze
kupata faida na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia kanuni bora za kilimo pamoja na
udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili.
Kwa manispaa ya Musoma zao la nyanya hulimwa na wakulima hulitegemea zao hili kama zao
la biashara kwa kuwa huwapatia faida kubwa ukilinganisha na mazao mengine ya mbogamboga.
Halmashauri ya Manispaa ya Musoma imelipa kipaumbele zao hili kwa kulichagu zao hili na
kuliweka kwenye mnyororo wa thamani kwa kutoa mafunzo ya kilimo bora cha zao la nyanya ili
wakulima waweze kulima zao hili kwa tija.