Kwa ufupi:
Ugonjwa wa Banana Xanthomonas wilt (BXW) umepewa jina lake kutoka kwa bakteria
wanaoambukiza na hatimaye kuua mgomba. Ugonjwa huo umeongezeka sana Uganda tangu
ulipopatikana kwa mara ya kwanza mwaka wa 2001 na sasa umeenea katika kanda yote. Aina zote
za migomba hushambuliwa ingawa matokeo ya utafiti yameonyesha uwezekano wa kupatikana kwa
aina sugu siku zijazo. Aina kuu ya usimamiaji kwa sasa ni kuzingatia usafi wa shamba: kupanda
mazao ya afya, kutumia zana safi za kukatia na kuondoa maua dume ili kupunguza kuathiriwa
kupitia wadudu wanaobeba bakteria wakati wanapofyonza utomvu. Ugonjwa wa BXW haupatikani
Afrika Magharibi; na ule ugonjwa mwengine mkubwa zaidi wa mnyauko bacteria duniani kote
unaosababishwa na Ralstonia solanacearum (ugonjwa wa Moko), haupatikani kote Afrika