Kwa ufupi:
Nchini Tanzania zao la nyanya hulimwa karibu katika mikoa yote hasa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mwanza, Dodoma, Tanga, Pwani na Mbeya. Nyanya ni zao la chakula na
biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana
haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze
kupata faida na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia kanuni bora za kilimo pamoja na
udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili.