Kwa ufupi:
Kutumia kilimo hai katika kilimo
cha ndizi kunachangia katika
uzalishaji endelevu na udhibiti wa
magonjwa na wadudu na huweza
kuleta mavuno mengi
Kulingana na Shirikisho la kimataifa la harakati za kilimo hai (IFOAM, 2008), Kilimo-hai
kinafafanuliwa kuwa ni “ mfumo wa uzalishaji ambao unaendeleza afya ya udongo, mifumo
ya ikolojia na watu. Kilimo hiki hutegemea kwenye michakato ya ki-ikolojia, bioanuwai na
mizunguko asilia ambayo inakubaliana na mazingira ya maeneo husika, badala ya kuingiza
pembejeo ambao zina athari mbaya. Kilimo hai kinajumuisha utamaduni, ubunifu na sayansi ili
kunufaisha mazingira tunayoshirikiana na kukuza mahusiano ya haki na maisha bora kwa wote
wanaohusika”.