Kwa ufupi:
Nyanya ni miongoni mwa mazao ya mboga yanayozalishwa nchini Tanzania.Nyanya imewekwa katika kundi la mboga za matunda sababu kuu ni kwamba tundalake ndiyo sehemu ya mboga inayotumika kwa chakula.Takwimu zinaonyesha kwamba nyanya inachangia asilimia 64 ya mazao yamboga na matunda yanayolimwa nchini Tanzania. Nyanya zinalimwa maeneo mengi nchini Tanzania japokua mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa kiasi kikubwa ni Morogoro, Iringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Singida, Tanga na Zanzibar.
Mkoa wa Morogoro ndiyo unaoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana.
Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira, kukosekana kwa masoko, wadudu, magonjwa na magugu sumbufu.