Ghala la Mkulima

Kilimo bora cha Mpunga

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

dc.contributor.author Kilasi, Newton
dc.date.accessioned 2022-04-12T10:57:56Z
dc.date.available 2022-04-12T10:57:56Z
dc.date.issued 2020-05-14
dc.identifier.uri http://10.10.11.5/xmlui/handle/123456789/577
dc.description.abstract Mpunga ni moja ya zao muhimu zaidi la chakula katika Afrika Mashariki. Nchini Tanzania mpunga unashika nafasi ya pili baada ya mahindi. Zao hili la chakula na biashara hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya, Morogoro, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Pwani, Dodoma, Mtwara na Lindi. Inakadiriwa kuwa asilimia 30-40 za mpunga hupotea baada ya kuvuna kila mwaka. Upotevu huu hutokana na teknolojia duni zinazotumika wakati wa kuvuna, kusafirisha, kukausha, kupura, kuhifadhi na kukoboa. Mvua ni chanzo kikuu cha maji kwenye kilimo cha mpunga. Viwango vya mahitaji ya maji katika kukua kwa mpunga hutofautiana miongoni mwa aina za mpunga. Ni kwa jinsi hii mpunga hupandwa katika mazingira mbalimbali kutegemea na mahitaji yake ya maji. Zipo aina tatu kuu za mazingira yanayolimwa mpunga kulingana na upatikanaji wa maji na hali ya mwinuko wa nchi. Mazingira haya ni kilimo cha mpunga wa mabondeni kinachotegemea mvua (72%), kilimo cha mpunga wa kwenye miinuko (20%) na kilimo cha mpunga cha umwagiliaji (8%). Kiasi cha mpunga kinachozalishwa nchini kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka kutoka tani 41,000 mwaka 1970 hadi tani 811,500 mwaka 1998. Ongezeko hili limetokana na kuongezeka kwa eneo linalolimwa mpunga na kwa kiasi kutokana na kuongezeka kwa miradi midogo ya umwagiliaji pamoja na matumizi ya tekinolojia bora za kilimo. Maeneo yanayolima mpunga kwa wingi Tanzania: ni Morogoro maeneo ya bonde la kilombero/Ifakara, Dakawa, Malolo; Mbeya: Kyela, Mbarali; Shinyanga: Kahama; Mwanza, Bonde la Ruvu mkoani Pwani. Na maeneo mengine mengi en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Sokoine University of Agriculture en_US
dc.subject Mpunga,Mbegu,Shamba, en_US
dc.title Kilimo bora cha Mpunga en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

kinaonekana kwenye vifungu vifuatavyo

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

Tafuta kwenye mkulima


Peruzi

My Account

Takwimu