Kwa ufupi:
Kitabu hiki kinatoa mwongozo wa mbinu bora za uzalishaji wa Zabibu kwa mkulima wa
kawaida, pia tumetumia lugha rahisi ili kumuwezesha mkulima kuelewa kwa urahisi, pia
kimetumia michoro mingi ili kumsaidia mkulima kuona kwa vitendo, na pia kimetumia
mazingira halisi ya Wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma.
Jitihada nyingi zimefanyika ili kuhakikisha Wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma wanalima
kisasa zaidi ili kujihakikishia mavuno bora na ya uhakika kipindi cha msimu wa mavuno.
Kutokana na utafiti uliofanyika na Taasisi mbalimbali inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya
Wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma wanalima kwa kutumia uzoefu tu na si kitaalamu kama
inavyotakiwa, hii inapelekea Wakulima wengi kutumia gharama kubwa katika uzalishaji wa zao
hili kwa kuwa wengi wao wanatumia uzoefu na si utaalamu, hivyo kupelekea Wakulima kupata
kipato kidogo ambacho hakilingani na uwekezezaji walioweka.
Hivyo kitabu hiki kitaainisha mbinu zote za msingi katika uzalishaji wa Zabibu ili kumpunguzia
mkulima gharama za uzalishaji, na pia kuendesha kilimo kibiashara zaidi.
Nimatumaini yangu kuwa kama Wakulima watazifuata mbinu hizi wataongeza uzalishaji wa zao
hili na hivyo kuwaongezea kipato zaidi.