Kwa ufupi:
Karanga ni zao lenye viini lishe vya protini na mafuta kwa wingi. Mabaki ya mimea ya
karanga pia yana viini lishe vya protini, hivyo ni chakula kizuri cha mifugo.Karanga pia huboresha rutuba ya udongo kwa kuongeza kiasili cha naitrojenikwenye udongo. Sifa hizi zinafanya karanga kuwa mmea bora katika kilimo cha kuchanganya au kuzungusha mazao hasa jamii ya nafaka.