Kwa ufupi:
Parachichi (Persea americana) ni mti, mrefu unaosemekana asili yake
ni Kusini Kati mwa nchi ya Mexico. Tunda la mmea, pia linaitwa parachi
(au avocado pear au alligator pear), ni asili ya mmea wa tunda kubwa
linalokuwa na mbegu kubwa inayokulikana kama "shimo" au "jiwe".
Parachichi kama yalivyo matunda mengi yenye virutubisho vya lishe
yana thamani kubwa ya kibiashara na kulimwa sehemu zenye ukanda
wa kitropiki na mediteranea duniani kwote. Kiwango cha hali ya afya ya
udongo unaofaa kustawi kwa parachichi ni kati ya pH 6.2 na 6.5..
Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC), Tanzania imeshuhudia uuzaji nje
ya nchi ukikua kwa CAGR ya asilimia (35%), kutoka mwaka 2013 mpaka
2017, ikikaribia tani za ujazo elfu 4.4 mwaka 2017 kutoka tani za ujazo elfu
1.4 mwaka 2013.
Nchini Tanzania, uzalishaji wa Parachichi unaanza kufahamika miongoni
mwa jamii huku mashamba mapya yakiendelea kufunguliwa maeneo
mbalimbali nchini. Mikoa kama ya Njombe, Iringa, Geita na hata mkoa
wa Kagera kumeshuhudiwa ongezeko la maeneo yaliyopandwa na
hutoa mavuno makubwa; aina inayopandwa kwa ajili ya soko la nje –
Hass na Fuerte. Mikoa mingine ambapo parachichi hulimwa ni Arusha,
Morogoro, Kilimanjaro, Mbeya, Songwe and Ruvuma. Parachichi
linahitajika sana kwenye soko la dunia kwa sasa na kuweza kuchangia
mapato ya fedha za kigeni na mapato kwa Serikali kama litasimamiwa
vizuri.
Mbali ya kuongezeka kwa ukubwa wa mauzo ya nje ya nchi, kuna hamu
ya Uwekezaji katika kuongeza thamani ya Parachichi. Kongani ya Ihemi
viko viwanda viwili, mkoani Iringa kipo Zalacado na mkoani Njombe kipo
Olivado.