Kwa ufupi:
Mwaka uliopita umekuwa na ongezeko la shughuli katika Idara ya Uboreshaji wa
zao la kahawa. Majaribio zaidi yameongezwa, mbegu chotara kuendeleza aina bora
zimezalishwa, na watafiti waliokuwa masomoni kwa Shahada ya Uzamili
wanakaribia kumaliza masomo yao na pia tulianza kazi ya kuzalisha miche kwa njia
ya chupa.Kazi zote zilizoongezeka zimefanywa kwa kutumia wafanyakazi wachache
waliopo Idarani ambapo ongezeko la kazi lilikuwa changamoto kubwa. Hapo
mbeleni, kuna umuhimu wa Idara kuendeleza kitaalamu Bw/Bi. Shamba waliopo na
kuajiri angalau wengine watatu ili kukabiliana na ongezeko la kazi.