Imetambulika ya kuwa ufugaji wa nyuki inaweza kuwapa watu wa mashambani njia ya kujipatia mapato zaidi. Ijapokuwa ufugaji wa nyuki sio rahisi kila wakati. Nyuki wanaweza kudunga mara nyingi bila kutarajiwa. Uvunaji wa asali inategemea mbinu nyingi kama vile hali ya anga na kwa kupata soko. Asali ya hali ya juu lazima uwe na ubora zaidi. Nta pia ni bidhaa ya muhimu na wakati mwingine huaribiwa.
Mwongozo huu wa shambani imetengenezwa ili kusaidia wakufunzi wanaofanya kazi katika Afrika kusini mwa Sahara. Picha yenye rangi ziko na maneno machache. Nakala hii pia inaeleza mbinu rahisi zinazohitajika kuanzisha biashara ya ufugaji wa Nyuki. Pia inatupatia mawazo au mbinu zinazohitajika kuanzisha ufugaji wa Nyuki kwa kutengeneza vyombo vyao wenyewe wakitumia vifaa vya kiasili. Natumaini kuwa hii itasaidia watu kuanzisha ufugaji wa nyuki kwa bei nafuu na labda kufanya majaribio na vitu vipya.
Picha hizi zinaonyesha kati ya njia nyingi ambazo watu hutumia kufuga nyuki. Hii inatarajiwa kuwezesha majadiliano na ushirikiano ili kusaidia watu kutatua shida zao wenyewe. Nakala hii inaegemea ufugaji wa nyuki kutumia mzinga wa ‘top bar’ lakini kuna mbinu nyingi na mawazo zinazoweza kutumika na wafugaji nyuki wa kitamaduni na wale wa kisasa wanaotumia mzinga wa fremu.
Inatarajiwa kuwa wakufunzi wataweza kutafsiri mbinu hizi kwa lugha ya kiasili. Shukrani kwa usaidizi wa Waterloo Foundation, kwani nakala nyingine itakuwa tayari ifikapo mwaka 2010. Hii itajumuisha mbinu za kisasa za ufugaji wa nyuki na mbinu za kutatua shida. Nakala ya maandishi pekee kwa wakufunzi pia inaweza kupatikana, kwa kutuma ombi kwa Pam Gregory ambayo inafafanua ‘sababu’ na ‘njia’ za ufugaji wa nyuki. Tuma barua pepe kwa:
[email protected]