Kwa ufupi:
Kuboresha lishe ni msingi katika kufanikisha malengo yote ya Maendeleo Endelevu. Uwepo wa utapiamlo sugu (udumavu) unadhoofisha maendeleo katika uhakika wa chakula, uboreshaji wa elimu, na afya bora ya mama na mtoto nchini Tanzania. Lishe duni ndio sababu kubwa ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania na inakadiriwa kugharimu serikali asilimia 2.6 ya Pato la Taifa kila mwaka. Upotezaji huu wa mapato uko katika sekta ya kilimo na husababishwa na ukuaji duni wa akili na mwili unaotokana na utapiamlo.Kulingana na Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya ya mwaka 2015-2016, takriban theluthi ya watoto wote chini ya miaka mitano wana udumavu na asilimia 14 wana upungufu wa uzito. Sababu kuu zinazoongoza kuleta utapiamlo ni ukosefu wa lishe mchanganyiko na bora kwa kila kaya, upatikanaji mbovu wa huduma za afya (pamoja na maji safi na salama, usafi wa mazingira), na mienendo duni ya lishe. Hali ya upungufu wa damu kwa mama ni shida nyingine kubwa nchini Tanzania, ikiwa na asilimia 57 ya wanawake wajawazito na asilimia 46 ya mama wanaonyonyesha wanaathiriwa.