Kwa ufupi:
Lishe bora ni muhimu kwa watoto wote hususan wenye virusi
vya UK1MWI kwa ajili ya ukuaji na maendeleo yao. Watoto
wanakua kwa haraka hivyo wana mahitaji makubwa ya chakula
ili kuwapatia virutubishi muhimu yaani nishati-lishe, protini,
madini na vitamini.
Watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI na wenye UKIMWI
wako katika hatari kubwa ya kupata utapiamlo kutokana na:
1. Ongezeko la mahitaji ya virutubishi hasa nishati-lishe.
2. Maradhi ya mara kwa mara,
3. Ulaji duni,
4. uyeyushaji na ufyonzwaji duni wa virutubisho mwilini.