xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.contributor.author | Msanga, H. P | |
dc.date.accessioned | 2020-11-10T07:11:21Z | |
dc.date.available | 2020-11-10T07:11:21Z | |
dc.date.issued | 2017 | |
dc.identifier.isbn | 978-9987-483-35-8 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/xmlui/handle/123456789/528 | |
dc.description.abstract | akwimu zinaonyesha kuwa eneo la misitu ya asili hapa Tanzania ni hekta (ha) 48,000,000 na misitu ya kupandwa ni ha 553,000. Inakadiriwa kuwa uharibifu wa misitu ya asili ni ha 403,000 kwa mwaka. Uharibifu huu mkubwa unasababishwa na mambo mengi hasa ongezeko la watu ambao shughuli zao zinasababisha kilimo cha kuhama hama, idadi ya mifugo iliyozidi uwezo wa eneo, uchomaji moto kiholela, upanuzi wa makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Athari za shughuli hizo ni pamoja na kukauka kwa vyanzo vya maji, uhaba wa mazao yatokanayo na miti, uharibifu wa mazingira na upoteaji wa bioanuwai. Ili kukabiliana na uharibifu huu, njia mojawapo ni kuongeza kasi ya upandaji miti na kudhibiti matumizi yake. Hili ni jukumu la kitaifa ambalo kila mwananchi anapaswa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake. Kabla ya kampeni ya kitaifa ya kupanda miti vijijini (Village Afforestation Programme) kuanza rasmi mwaka 1970, kwa kiasi kikubwa jukumu la kupanda miti na kusimamia misitu lilikuwa la serikali kupitia Idara ya Misitu na Nyuki. Wakati wa kampeni hiyo, wananchi na taasisi mbalimbali zilihusishwa na kuhimizwa kushiriki katika upandaji miti kwa ajili ya matumizi mbalimbali chini ya dhana ya “Misitu ya Jamii” (Community Forestry). Kutokana na Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Taifa ya Hifadhi za Mazingira ya mwaka 2004 na Programu mbalimbali za kuhamasisha upandaji miti kila mwaka, ni dhahiri kuwa Serikali inahimiza wananchi na taasisi zishiriki kikamilifu katika suala la kupanda miti. Upandaji miti unaweza kufanywa na taasisi za serikali, makampuni ya wawekezaji, vikundi vya jamii, shule na hata watu binafsi. Miti inaweza ikapandwa peke yake ikawa msitu, mti mmoja mmoja katika shamba, kuzunguka shamba, katika maeneo ya makazi, kando kando ya barabara na penginepo kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu. Kwa kuzingatia umuhimu wa kupanda miti na kuitunza, mwaka 1999 Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa kupitia Mradi wa Taifa wa Mbegu za Miti (National Tree Seed Programme - NTSP) sasa Wakala wa Mbegu za Miti (Tanzania Tree Seed Agency - TTSA) ilichapisha kitabu kiitwacho “Aina ya miti inayofaa kwa maeneo mbali mbali ya Tanzania Bara na maandalizi ya bustani ya miche”. Kitabu hicho kilitokana na mada iliyotolewa na Dkt. Heriel Msanga katika semina ya Wakuu wa Mikoa iliyofanyika huko Dodoma tarehe 15, Aprili 1999 | en_US |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | Wakala wa Mbegu za Miti, Wizara ya Maliasili na Utalii | en_US |
dc.subject | Miti | en_US |
dc.subject | Misitu | en_US |
dc.title | MWONGOZO WA UPANDAJI NA UTUNZAJI WA MITI YA MBAO, MATUNDA NA MATUMIZI MENGINE, TANZANIA | en_US |
dc.type | Book | en_US |