Kwa ufupi:
Chakula bora kwa Nguruwe ni moja ya suala muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa Nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha Nguruwe kinagharimu kama asilimia sabini ya garama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya matatizo mengi yanayosababisha tija na ufanisi duni wa uzalishaji wa Nguruwe yanatokana na lishe duni. Lakini kama wakipatiwa lishe bora, tija na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.