Kwa ufupi:
Baada ya miezi 6 watoto wanahitaji aina nyingine ya vyakula pamoja
na maziwa ya mama ili kuwafanya kuendelea kukua vyema. Aina
mbali mbali za vyakula vitamsaidia mtoto wako katika njia mbali
mbali. Wape watoto wako mchanganyiko wa vyakula hivi mbali mbali
kila siku. Vyakula hivi vinaweza kupikwa kulingana na mahitaji.