Kwa ufupi:
Upungufu waa madini ya joto mwilini ni tatizo kubwa la kiafya hapa Tanzania. Idadi ya watu wanaoathirika inakadiriwa kuwa milioni 5.6 au asilimia 25 ya watu wote.
Madini ya joto hupatikana ardhini na huchukuliwa na aina zote za viumbe (mimea, wanyama) na maji, vinavyopatikana katika eneo hilo. Kupitia katika vyakufa madini hayo huingia kwenye mwili wa binadamu. Kutokana na mlolongo huo iwapo ardhi ya eneo fulani ina upungufu wa madini ya joto binadamu nao kupungukiwa na hatimaye
kupatwa na madhara. Sababu za upungufu wa madini ya joto ni zaidi ya moja, lakini kubwa na ya muhimu niile ya kijiografia. Sehemu za miinuko, kwa miaka mingi tangu kuumbwa kwa dunia, zimepoteza madini ya joto ambayo huchukuliwa na maji (mvua, mito, mafuriko n.k.) na kupelekwa nyanda za nchini yaani bondeni, baharini na kwenye maziwa. Nd'iyo maana tatizo ni kubwa sana katika mikoa yenye miinuko na siyo katika ukanda wa pwani.