Kwa ufupi:
Magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza yanayohusiana na mtindo wa maisha yamekuwa yakiongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Awali, magonjwa haya yalikuwa yakiwaathiri watu wenye rika mbalimbali hasa wenye umri mkubwa (> miaka 45) lakini kwa sasa magonjwa haya yanazidi kuathiri watu wenye umri mdogo wakiwemo watoto. Magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza huwa yanachukua muda mrefu kujitokeza. Magonjwa sugu makuu matano yasiyo ya kuambukiza – kisukari, shinikizo kubwa la damu, magonjwa ya moyo, saratani, magonjwa sugu yasiso ya kuambukizwa yanajitokeza kwa wingi kwenye nchi zenye uchumi mdogo na wa kati.