Kwa ufupi:
Viazi Vitamu ni zao muhimu nchini Tanzania na linashika nafasi ya pili likitanguliwa na zao la mihogo katika mazao ya mizizi. Viazi vitamu vinalimwa maeneo mengi ya Tanzania na kati ya wazalishaji wakubwa ni kanda ya kati ikiwemo Mikoa ya Dodoma na Singida.
Kwa asili wakulima wamezoea kulima viazi vitamu vyenye rangi nyeupe au ya maziwa kwa ndani.
Hata hivyo kuna vyenye rangi ya karoti kwa ndani ambavyo vina vitamini A kwa wingi. Kutokana na kuwa na Vitamini A kwa wingi vinaitwa viazi lishe