Kwa ufupi:
Ufugaji wa mende ni ufugaji unaokua kwa kasi sana hapa nchini, hii ni kutokana na faida zinazoaminika kupatikana kwa mende.Hivyo kwa namna hii kasi ya ufugaji inaongezeka, kunauwezekano mkubwa sana kwa wafugaji wengi kuingia katika ufugaji huo ha hivyo kuongezeka kwa ushindani.Ufugaji wa mende hauna masharti mengi sana na pia hua na gharama ndogo katika kufuga licha ya kuaminika kua na faida.
Kuna Aina zaidi ya 400 za mende duniani na katika hizo aina 30 pekee ndio zinapatikana katika makazi ya watu, lakini katika hizo aina 4 ndio ambazo ni sumbufu majumbani. Ila mende ambao wamefanyiwa utafiti kwaajiri ya chakula cha kuku, binadamu na hata kutengeneza dawa za urembo ni mende wa Asia ambao wamechanganywa katika aina 3 ili kuweza kupata aina moja bora zaidi (breeding) na aina hizi ni mende wa Asia, Ujerumani na Marekani na kwa kitaalamu mende huyu huitwa diloptera punctuate.