Kwa ufupi:
Pilipili mbuzi ni zao ambalo linaweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida
nzuri mkulima. Zao hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua angalau kiasi cha
masaa 6 kwa siku.
Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili, undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji.
Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa PH ni chini ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya udongo imefka 8 onana na wataalam wa kilimo wakusahuri namna ya kuipunguza.