Kwa ufupi:
Mfumo wa ulaji unaotumika katika vijiji hivi umegawanyika
katika sehemu nne ambazo ni:
1. Baba kula pamoja na watoto wa kiume bila kubagua
umn
2. Mama kula peke yake
3. Mama kula na watoto wa kike bila kubagua umri
4. Watoto wa jinsia zote kula pamoja bila kubagua umri
Pamoja na mfumo huu wa ulaji bado kuna athari zitokanazo
na utayarishaji mbaya wa chakula ambao ni pamojana
kutokula vyakula vya mchanganyiko kutoka mafungu makuu
matatu ya chakula. Mahmgu hayo ni vyakula aina ya
nafaka/mizizi vinavyotia nguvu mwilini tuweze kufanya kazi
za nguvu kama kulima, kutembea mwendo mrefu, kukokota
plau/kuendesha trekta, kubeba zege n.k. Vyakula hivyo ni
pamoja na nafaka kama mahindi, ulezi, mtama, ngano na
mpunga na mizizi ni kama muhogo, viazi vitamu, viazi
mviringo, magimbi, viazi vikuu, n.k.. Vyakula vya protini
hujenga miili yetu kwa maana ya kurudishia upya sehemu
zinazochakaa, kwa mfano misuli kwa watu wazima, kucha,
kidonda kupona na kufunga haraka tunapopata majeraha.
Kwa upande wa watoto wadogo ambao bado wanakua
huwasaidia wakue haraka, Vyakula hivi vimegawanyika
katika aina mbili: vile vya asili ya nyama ambavyo ni nyama,
samaki, maziwa, mayai na wanyama wa porini, na vile vya
asili ya mimea, ni kama maharage, choroko, kunde, mbaazi.
njegere na njugu mawe. Vyakula vingine ni kundi la
mbogamboga na matunda. Hivi husaidia miili yetu
isishambuliwe na maradhi. Vyakula hivyo ni majani ya kunde, majani ya maboga, kisamvu, bamia, karoti, mchicha,
mwidu, delega, mnavu, n.k. Matunda ni pamoja na mapapai,
mapera, machungwa, embe mafuta n.k. na yale ya asili kama
ukwaju, ubuyu, n.k.