xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.contributor.author | Kinabo, Prof. J. L. | |
dc.contributor.author | Mnkeni, Dr. A. | |
dc.contributor.author | Nyaruhucha, Dr. C. | |
dc.contributor.author | Msuya, Dr. J. | |
dc.contributor.author | Chale, Bi. F. | |
dc.date.accessioned | 2022-06-27T06:42:29Z | |
dc.date.available | 2022-06-27T06:42:29Z | |
dc.date.issued | 2005-02-09 | |
dc.identifier.isbn | 9987- 422 - 07-1 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/xmlui/handle/123456789/654 | |
dc.description.abstract | Mfumo wa ulaji unaotumika katika vijiji hivi umegawanyika katika sehemu nne ambazo ni: 1. Baba kula pamoja na watoto wa kiume bila kubagua umn 2. Mama kula peke yake 3. Mama kula na watoto wa kike bila kubagua umri 4. Watoto wa jinsia zote kula pamoja bila kubagua umri Pamoja na mfumo huu wa ulaji bado kuna athari zitokanazo na utayarishaji mbaya wa chakula ambao ni pamojana kutokula vyakula vya mchanganyiko kutoka mafungu makuu matatu ya chakula. Mahmgu hayo ni vyakula aina ya nafaka/mizizi vinavyotia nguvu mwilini tuweze kufanya kazi za nguvu kama kulima, kutembea mwendo mrefu, kukokota plau/kuendesha trekta, kubeba zege n.k. Vyakula hivyo ni pamoja na nafaka kama mahindi, ulezi, mtama, ngano na mpunga na mizizi ni kama muhogo, viazi vitamu, viazi mviringo, magimbi, viazi vikuu, n.k.. Vyakula vya protini hujenga miili yetu kwa maana ya kurudishia upya sehemu zinazochakaa, kwa mfano misuli kwa watu wazima, kucha, kidonda kupona na kufunga haraka tunapopata majeraha. Kwa upande wa watoto wadogo ambao bado wanakua huwasaidia wakue haraka, Vyakula hivi vimegawanyika katika aina mbili: vile vya asili ya nyama ambavyo ni nyama, samaki, maziwa, mayai na wanyama wa porini, na vile vya asili ya mimea, ni kama maharage, choroko, kunde, mbaazi. njegere na njugu mawe. Vyakula vingine ni kundi la mbogamboga na matunda. Hivi husaidia miili yetu isishambuliwe na maradhi. Vyakula hivyo ni majani ya kunde, majani ya maboga, kisamvu, bamia, karoti, mchicha, mwidu, delega, mnavu, n.k. Matunda ni pamoja na mapapai, mapera, machungwa, embe mafuta n.k. na yale ya asili kama ukwaju, ubuyu, n.k. | en_US |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | TARP II - SUA PROJECT | en_US |
dc.subject | Mapishi ya mbogamboga | en_US |
dc.subject | Mapishi ya pilau | en_US |
dc.subject | Mapishi ya Vitafunwa | en_US |
dc.title | Mapishi: Vyakula vinavyozalishwa katika mkoa wa Morogoro | en_US |
dc.type | Book | en_US |